Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu
Mkoa
wa Simiyu umejipanga kimkakati katika kuhakikisha unaongeza ufaulu
kwenye Elimu na kuwa miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri Kitaifa kutoka
mahali ulipo sasa, kwenda kwenye nafasi ya tarakimu moja(single digit)
yaani nafasi ya kwanza hadi ya tisa.
Hayo
yalibainishwa katika kikao maalum kilichofanyika jana Mjini Bariadi
kati ya Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya,
Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo
yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, kilichofanyika
jana Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewataka walimu pamoja na
watendaji wengine wa idara ya Elimu kuongeza bidii katika maeneo yao ili
waweze kuufikisha mkoa katika nafasi ya tarakimu moja (single digit)
kwa kuwa sababu, uwezo na nia ya kufika hapo ipo.
“Watu
wa Sekta ya elimu Ombi langu kwenu wakati tukiwa tunajipongeza kuwa wa
14 katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017 tudhamirie kuongeza bidii
ili tuingia kwenye ‘single digit’, sababu za kuingia kwenye ‘single
digit’ zipo, uwezo upo kwa kuwa ninyi mpo na nia ya Simiyu kuonekana juu
tunayo” alisema Sagini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi..
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na walimu mahiri kwenye masomo mbalimbali katika Mitihani ya Kitaifa mwaka 2017 mara baada ya kikao cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na walimu hao, kumalizika jana mjini Bariadi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...