Na Fredy Mgunda,Mufindi.
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo Mgimwa alisema kuwa ametoa mabati 280, mifuko 310 ya saruji, rangi za maji na mafuta na sim tenki la lita mia tano (500) za kuhifadhia maji.
“Nilifanya ziara katika vijiji vya kata hizo nikaona wananchi wanavyojitoa kuboresha sekta ya elimu na mimi kama mbunge wao nikaamua kuwaunga mkono kwa kuchangia vifaa hivyo” alisema Mgimwa
Mgimwa alizitaja kata zinazonufaika na msaada huo ni kata ya Mapanda, Kibengu, Ihanu na Sadani na akavitaja vijiji vinavyonufaika na msaada huo kuwa ni pamoja na Ihimbo, Ukami na Chogo katika kata ya Mapanda; na Kipanga, Igeleke, Kibengu, Usokami na Igomtwa katika kata ya Kibengu.
Vingine ni kijiji cha Lulanda katika kata ya Ihanu na katika kata ya Sadani Mgimwa sehemu ya msaada huo inakwenda kusaidia ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mgalo.Aidha Mgimwa alisema kuwa ataendelea kusaidia maendeleo kwenye vijiji ambavyo vinafanya maendeleo katika jimbo lake
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikabidhi sim tanki ya lita 500 kwa viongozi
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...