Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

WANASHERIA zaidi ya 100 wameanza kupitia na kuchambua malalamiko mbalimbali ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa 
lengo la kuhakikisha yanapatiwa majibu.

Hatua hiyo inatokana na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika 
kwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda na kisha kutoa malalamiko 
kuhusu mambo mbalimbali.

Kutokana na malalamiko hayo Makonda aliaahidi kuyashughulikia na sasa timu hiyo ya wataalamu wa masuala ya sheria wameanza jukumu la kupitia malalamiko ya wananchi hao na kisha kutafuta ufumbuzi wake wa kisheria.

Akizungumza jana , Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Fabiola Mwingira amesema wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko hayo na baada ya hapo wataanza 

kuyasikiliza kwa kukutanisha pande zote mbili kwa maana ya mtoa malalamiko na anayelalamikiwa."Wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko ya wananchi kuanzia leo hadi Machi 9 mwaka huu na lengo kila mwananchi aliyepeleka malalamiko yake basi yapate 
ufumbuzi.

"Malalamiko wanayoyashughulikia ni yale ambayo hayako mahakamani na yaliyo mahakamani basi yatabaki huko huko yapatiwe ufumbuzi na tayari wamewaandikia barua wahusika,'amesema Mwingira.

Amefafanua baada ya wanashera hao kumaliza kusikiliza malalamiko hayo, watatoa ushauri wa kisheria ambao utamuwezesha sasa Mkuu wa Mkoa kutoa uamuzi.Pia amesema utoaji majibu ya kero za wananchi hao awamu ya pili ,majina yatabandika kwenye geti la ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,hivyo wananchi watatangaziwa siku na saa.
WANASHERIA wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Fabiola Mwingira aliyevaa blauzi yenye mistari na Georgia Kamina wa kwanza kulia, wakitoa maelekezo kwa sehemu ya jopo la wanasheria ambao jana wameanza kuchambua na kupitia malalamiko yote ambayo yamewasilishwa na wananchi wa mkoa huo ili yapatiwe majibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...