Mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi umezindua maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.4 kwenye shule ya sekondari Bugisha iliyopo katika kata ya Mondo wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu kuchangia katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.
Maktaba hiyo imezinduliwa leo Alhamis Februari 8,2018 na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba na kuhudhuriwa pia na Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Benedict Busunzu.
Hii ni maktaba ya pili katika wilaya ya Kahama kuzinduliwa na mgodi huo ambapo mwaka 2017 mgodi wa Buzwagi ulianzisha maktaba ya jamii katika kata ya Kagongwa ili kutoa rasilimali za elimu ya aina mbalimbali kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Akizungumza wakati uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu,Benedict Busunzu maktaba hiyo itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka jamii inayouzunguka mgodi wa Buzwagi.
Alisema kupitia mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha. Katikati ni Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu.Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akifuatiwa na diwani wa kata ya Mondo Kija Peja
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba akiangalia vitabu katika maktaba ya shule ya sekondari Bugisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kahama,Underson Msumba na Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu wakisoma vitabu ndani ya maktaba ya shule ya sekondari Bugisha
Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bugisha lililoboreshwa na mgodi wa Buzwagi kwa kushirikiana na Read International - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...