Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam limetangaza vita kwa wale wadaiwa sugu kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada. Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga wakati akizindua kampeni ya kukusanya madeni kwa wateja wao.
"Leo tunazindua kampeni ya kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu wote wa SIDO hatutakuwa na huruma juu ya hili maana hawa ndiyo wanarudisha maendeleo ya shirika nyuma, kuna waliokopa, walipanga kama haujalipa deni lako ujue tunakupa siku 14 tu baada ya hapo sheria itachukua mkondo wake," amesema Mkurugenzi Maganga.
Meneja Macdonald Maganga amesema wadaiwa ni wale waliopewa maeneo maalumu ya viwanda kwa ajili ya kufanyia kazi zao na waliopatiwa huduma ya fedha kwa mkopo na kushindwa kurejesha kwa wakati. “Kuna ambao wamekaa miaka mingi au miezi mingi bila kurejesha fedha kwetu kama shirika inatuathiri kwa sababu hatuwezi kuwahudumia wengine,” amesema Maganga. Maganga amesema wanadai jumla ya sh. milioni 350 kutoka kwa wadaiwa zaidi ya 77.
Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akitoa uamuzi wa wao kuwaweka kampuni ya udalali ya Yono Auction kwa ajili ya kwenda kukamata wadaiwa sugu wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela akitoa tamko la siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada kufidia deni.
Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akiongoza wafanyakazi na viongozi wa Yono kupita mlango kwa mlango wakati wakizundua kampeni ya kudai madeni "LIPA DENI LAKO SIDO, KUWA MZALENDO'.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...