Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu umezindua na kukabidhi maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.6 kwenye shule ya sekondari Bulyanhulu iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani wa Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.
Maktaba hiyo imezinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Msalala Bw , Simon Berege na kuhudhuriwa na kaimu Meneja mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Elias Kasitila.
Akizungumza wakati uzinduzi huo, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi Bulyanhulu,Elias Kasitila alisema wakati wakitafakari namna ya kuinua taaluma ya wanafunzi waliona ni vyema wakaimarisha usomaji wa wanafunzi kwa kuwekeza kwenye maktaba ambayo itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka kwa jamii inayouzunguka mgodi huo.
Alisema kupitia mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba ambayo itawasaidia wanafunzi na walimu kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala ,Simon Berege akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu. Kaulia ni kaimu Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Elias Kasitila.Na katikati ni Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi .
Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu lililoboreshwa na mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na Read International .
Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akionesha sehemu ya kuangalia orodha ya aina za vitabu vilivyopo katika maktaba kwa mkurugenzi wa halmashauri ya msalala , Simon Berege .


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...