Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) imefanya maboresho ya Kanzidata na mfumo wa usajili wa vizazi na kifo kupitia mradi wa maboresho ya miundombinu ya  Tekknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa  Sifuni Mchome amesema kuwa lengo kuu la maboresho ni kuwezesha matukio ya vizazi na vifo kufanyika kwa ufanisi zaidi na kuwa karibu na wananchi katika  kuimarisha miundombinu ya usajili, krahisisha usafirishaji taarifa, uhifadhi wa taarifa pamoja na matumizi ya taarifa za ndani na nje ya Wakala.

“Maboresho ya mfumo wa usajili yamezingatia mahitaji ya mkakati wa kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu wenye lengo la  kuboresha usajili wa matukio muhimu” amesema.

Amesema maeneo yaliyolengwa katika mradi huo ni kama yafuatavyo ni kuboresha miundombinu ya kanzidata , kuweka vituo 60 vya majaribio na madawati manne ya usajili  wa RITA  katika Makao Makuu , Maboresho ya mfumo wa kielektronikI wa usajili ,maboresho ya mfumo wa utafutaji wa taarifa za zamani na kuweka mfumo maalum wa kutoa namba za kuzaliwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya mfumo mpya wa usajili  wa Wakala wa Usajili, ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kutumia TEHAMA wakati alipofanya ziara katika wakala huo leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili ,ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson akitoa ufafanuzi juu ya mfumo wa usajili wa vizazi na vifo kupitia mradi wa maboresho ya Miundombinu wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome  alipofanya ziara katika wakala huo leo jijini Dar es Salaam.
Watendaji na Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano  wa  Wakala wa Usajili, ufilisi na Udhamini (RITA) leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...