Na Karama Kenyunko , Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul “Diamond Platinumz" mapema leo asubuhi amefika katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Ustawi wa Jamii kwenye mahakama ya watoto kwa ajili ya usuluhishi juu ya matunzo ya mtoto wake aliyezaa na mlimbwende Hamisa Mobeto.

Alianza kuingia Diamond akafuatiwa na Hamisa baada ya muda kidogo ambapo walikaa kwa zaidi ya saa moja. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza usuluhushi huo, Diamond alisema,

“Kiasi cha pesa tunavyoviandika kama kama hivi, tunazungumza tu, lakini watoto hawahitaji mahitaji mengi, wakati mwingine mtoto wako una uwezo wa kumpa hadi Shilingi milioni 100 na huwezi kusema simpi kwa sababu niliandikisha nitampa Laki Moja haimsaidii”.

Alisema wao kama wazazi wameweka mazingira mazuri ya kumlea mtoto wao kwa kadri ya uwezo wataokapata, kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora wakipata watakula nae wakikosa watalala.
Alipohojiwa baada ya kumalizika kwa usuluhishi, wakili wa Hamisa Mobeto,Walter Goodluck amesema, "leo tulikuja kwa usuluhishi na wamesuluhishwa Ila sasa wamesuluhishwa nini na nini hilo tutalijua badae", amesema

Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akifika katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto.

Hamisa Mobeto akiwa
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul ‘Diamond Platinumz’ akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka ustawi wa jimii kwa ajili ya kwaajili ya usuruhisho wa matunzo ya mtoto wao aliyezaa na Hamisa Mobeto leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...