Serikali imesema iko tayari kupokea ushauri wa namna bora ya kuimarisha utendaji wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza Taasisi hiyo kwani bado inahitajika na madhumuni ya kuanzishwa kwake yana tija kwa Taifa.

Akizungumza wakati akijibu Hoja za Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Waziri wa Elimu Sayansi na Teknplojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika hivyo Serikali inaangalia namna ya kuiboresha na si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

“ Taasisi ya Elimu ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wale waliokosa katika mfumo rasmi na pia kutoa mafunzo endelevu hivyo bado kuna umuhimu wa kuendeleza Taasisi hii” Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Akifafanua Prof. Ndalichako amesema kuwa Taasisi hiyo inaweza kuimarishwa zaidi ili kuendana na mahitaji ya sasa ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha na kukuza kiwango cha elimu nchini.

Akizungumzia mikakati yakuimarisha elimu nchini Profesa Ndalichako amesema kuwa kwa sasa Serikali inafanya ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini, vyuo vya Ualimu, na Ujenzi wa maktaba yakisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja hiyo ikiwa ni sehemu ya miradi yakuboresha elimu inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yalipendekeza kuwa TEWW ivunjwe ambapo Serikali imesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika na ina tija hivyo kitakachofanyika ni kuiboresha zaidi ili kukuza elimu hapa nchini na Si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

Taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 139 ya mwaka 1989 na iko chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknoloji.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akionesha kwa wabunge baadhi ya Vitabu vyenye ubora unaotakiwa kwa matumizi ya wanafunzi ikiwa ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha elimu nchini ambapo pia alibainisha kuwa Serikali haitaivunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima badala yake inaangalia namna bora yakuimarisha Taasisi hiyo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa wabunge wakati akijibu hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni Mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...