Wakazi waishio jirani na Pori la Akiba la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa mkoani Dodoma, wameiomba Serikali iwarejeshee eneo la kilometa 12 kuanzia kwenye vijiji vyao kwenda ndani ya Pori hilo ambalo wanadai limechukuliwa kinyemela na Wizara ya Maliasili na Utalii na kuathiri maisha yao yanayotegemea kwa kiasi kikubwa kilimo na ufugaji.

Wakazi wa vijiji vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko, wametoa maombi hayo mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipofanyaziara katika vijiji hivyo vinavyozunguka Pori hilo la Akiba ili kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya Pori hilo na wananchi wanaolizunguka.

Wananchi na viongozi wa vijiji hivyo wameeleza kuwa uwekaji wa mipaka ya Pori hilo haukuwa shirikishi na kwamba maeneo makubwa ya vijiji yaliyokuwa yakitumiwa na wananchi kwa shughuli zao za kilimo, ufugaji na makazi yametwaliwa na kusababisha mgogoro huo.

Malalamiko mengine ya wananchi hao ni kunyanyaswa na watumishi wa Pori la Akiba Mkungunero kwa kupigwa, kunyang'anywa mifugo yao, na baadhi yao kudai kuumizwa na baadhi ya wenzao kuuawa kwa risasi na askari wanaolinda Pori hilo.

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji, ameiomba Serikali kutumia busara na kurejesha eneo lililochukuliwa kimakosa kutoka kwa wananchi ili waweze kujiendeleza kiuchumi na kuishi kwa amani na utulivu.

"Najua wewe ni mwadilifu ndio maana umeaminiwa na Mhe. Rais, najua utawatendea haki wananchi wa vijiji hivi ili nao wajione ni wananchi halali katika Taifa lao huru la Tanzania tukienda hatua kwa hatua bila kuvunja sheria za nchi" alisisitiza Dkt. Kijaji

Amefafanua kuwa maeneo yaliyochukuliwa na Pori hilo yalikuwa yakitumiwa na wananchi kwa muda mrefu na kwamba mchakato wa kupandisha hadhi eneo hilo kutoka Pori Tengefu hadi kuwa Pori la Akiba la Mkungunero haukuwashirikisha wananchi.
 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikengwa, Nade Laida, akibubujikwa machozi wakati wa mkutano kati ya wanakijiji na msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mwanamke huyo ni mmoja wa waathirika wa mgogoro baina ya Pori la Akiba Mkungunero na wananchi wa vijiji vinavyozunguka pori hilo.
 Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Keikei Tangini ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiwa ameshikilia bango linaloeleza kuwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero imesogezwa kwenye kijiji chao.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati)  akizungunza wakati wa mkutano ulioitishwa na Waziri wa Maliaasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala katika kijiji cha Keikei Tangini ili kusikiliza malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Pori la akiba Mkungunero kuhusu kumegwa kwa maeneno yao na Pori hilo, wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...