Kampuni ya Star Media (T) Ltd inayomiliki chapa ya StarTimes, jana katika Siku ya wapendanao iliwapatia fursa wateja wao kupata chakula cha jioni na wapenzi wao katika mgahawa wa kifahari wa Akemi, Posta jijini Dar es Salaam.
 StarTimes ambayo kwa wiki kadhaa iliwapatia nafasi wateja wake kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii kutuma picha wakiwa na wapenzi wao ili kujipatia nafasi hiyo adhimu ya kupata chakula cha jioni pamoja. Katika picha zote zilizotumwa na wateja wa StarTimes katika kurasa zao za mitandao ya kijamii, watano walibahatika kuchaguliwa na baadaye walipatiwa taarifa jinsi ya kufika kwenye mgahawa kwa ajili ya zawadi maalum.
Kabla ya kupelekwa mgahawani wapenzi hao walipata nafasi ya kutembelea ofisi za makao makuu ya Star Media (T) Ltd zilizopo Bamaga, Barabara ya Bagamoyo, Dar es Salaam, na kujionea jinsi ambavyo StarTimes hufanya kazi kila siku, miongoni mwa ofisi walizotembelea ni kituo cha Simu (Call Centre), Chumba cha Kurushia matangazo na Duka la vifaa mbalimbali vya StarTimes.
Wapendanao hao baadaye walipelekwa mgahawani kwa ajili ya Chakula cha jioni. Yote ikigharimiwa na kampuni ya StarTimes katika kuonyesha upendo kwa wateja wake katika Siku ya Wapendanao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...