Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza
jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mipango ya
Serikali ya kuendeleza kiwanja cha Ndege Mwanza kwa kuiboresha
miundombinu ili kiwanja hicho kiwe cha Kimataifa, wakati alipokagua
maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki
mbili kwa Mamlaka ya Viwanja Ndege Nchini (TAA), kukusanya fedha za
madeni ambayo inadai kutoka kwa watoa huduma mbalimbali katika viwanja
vyote vya ndege ili ziweze kutumika kuendeleza miundombinu.
Kauli hiyo ametoa jijini Mwanza, baada kukagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha ndege na hali ya uendeshaji katika kiwanja hicho ambapo amebaini kuwa kuna madeni ambayo yanaweza kulipika na kuweza kurahisisha shughuli za kiuendeshaji ikiwemo kujenga uzio ili kuongeza usalama kiwanjani hapo.
"Nataka TAA mkusanye madeni yote mnayodai, fedha hizi zikipatikana zinaweza kutumika kujenga uzio kwa ajili ya kulinda usalama wa uwanja ili wananchi wasiweze kuvamia na pia usalama wa ndege zinazoruka na kutua", amesisitiza Prof. Mbarawa.

wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akikagua maendeleo ya ujenzi barabara ya Pasiansi hadi Airport KM 4.6
inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza.
Amefafanua kuwa kama Taasisi hizi zikikusanya madeni na watoa huduma wakalipa kodi kwa wakati kutasaida Serikali kuboresha maendeleo ya miundombinu.
Kuhusu maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho. Prof. Mbarawa amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi ambapo kwa sasa umefikia asilimia 60.
Ameongeza kuwa ujenzi huo unategemewa kumalizika mwezi Julai mwaka huu na utagharimu kiasi cha shilingi takribani bilioni 94.
Aidha amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria mara miradi inayoendelea kukamilika.
Muonekano
wa eneo la kuegesha ndege ambalo ni moja ya utekelezaji wa mradi wa
upanuzi na uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza.
Naye Msimamizi wa Kiwanja hicho ambaye ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mwanza, Mhandisi Joseph Mwami, amesema kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kuongoza ndege, eneo la maegesho na njia za kuruka na kutua ndege
Mhandisi Mwami, amefafanua kuwa njia ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja hicho imeongezwa urefu wa mita 500 ili kuifanya kufikia urefu wa KM 3.5 ili kuwezesha ndege kubwa za kimataifa kuweza kutua na kuruka katika kiwanja hicho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...