Madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo Mkoani Pwani ,wakifuatilia kikao cha bajeti cha baraza la madiwani huko Lugoba.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo Mkoani Pwani ,ambae pia ni diwani wa kata ya Talawanda Saidi Zikatimu akizungumza katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani huko Lugoba .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
WAKAZI wa Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani, wataabika na kero ya ukosefu wa maji safi na salama takriban miezi mitatu sasa. Kufuatia kero hiyo baraza la madiwani la halmashauri ya Chalinze, limemuangukia rais Dk. John Magufuli kwa kumuomba aende kujionea mradi wa maji awamu ya tatu WAMI-CHALINZE ambao umekwama na kusababisha wananchi kukosa neema hiyo ya maji.
Madiwani hao wamesema Rais, ndiye mwenye mamlaka za mwisho kwani Waziri Mkuu alishafika kujionea mradi huo ambapo mkandarasi aliongezewa muda lakini mkataba umekwisha na hakuna kilichofanyika.
Wakitoa kilio hicho, wakati wa kikao cha kupitisha bajeti, baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa Talawanda ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Saidi Zikatimu alisema kuna kila sababu serikali ikaingilia kati na kutoa tamko ili kurejesha imani kwa wananchi. Alieleza tatizo hilo ni kubwa kwani zipo baadhi ya shule hazina maji safi na salama na wanahofiwa wanafunzi kupata magonjwa ya mlipuko.
"Maji ni tatizo mradi wa WAMI -CHALINZE, kamati ya fedha tulishaenda lakini majibu ya meneja wa CHALIWASA Christer Mchomba hayakuturodhisha "
"Baraza hili linaimani na Mh.Rais jambo hilo lichukuliwe ufumbuzi wa haraka zaidi ya miezi miwili ama mitatu hakuna maji, serikali itoe tamko kuhusiana na mradi huo "; alisema Zikatimu .
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...