Mfanyabiashara maarufu mkoani Kigoma, Carole P. Mtei amefariki tarehe 04/02/2018 katika hospitali ya Rabininsia, Tegeta jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa ykimsumbua. 

Mwili wa Marehemu Mtei unatarajiwa kuagwa leo Alhamisi 08/02/2018 katika Hospitali ya Lugalo na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwao Marangu, Moshi kwa Mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi 10/02/2018. habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Mtei popote pale walipo.
Neno: 
2 Timotheo 4: 7 
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.
Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu - Amin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...