Na Woinde Shizza,Kilimanjaro

IMEELEZWA kuwa teknolojia mpya itaanza kutumika kwenye hifadhi za Taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya Serikali kwa lengo la kupambana na ujangili hasa maeneo ambayo yameathirika zaidi.

Hivyo maofisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini watatumia teknolojia hiyo kukomesha jangili.

Hayo yamesemwa leo  na maofisa wa Wanyamapori,Maliasili,Ulinzi na Uhifadhi was mazingira katika hiadhi za Taiga na mapori ya akiba ya wanyama ya Serikali nchini.

Maofisa hao walisema matumizi ya simu na kompyuta zenye programu ya smart ambayo hutumiwa kuainisha maeneo hatarishi kwa ujangili na uvunaji holela wa miti yanaweza kuwekewa alama maalum za kitaalam na kuimarisha ulinzi zaidi.

Ofisa wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka, Rudolf Philemon amesema matumizi ya teknolojia hiyo yatasaidia kukabiliana na kupunguza vitendo vya kijangili.Pua uvunaji haramu wa misitu na kurahisisha mbinu za kuwakamata majangili.

Rudolf amesema kwa kutumia program hiyo ipasavyo inatarajia kupunguza vitendo vya ujangili katika Hifadhi za taifa na mapori ya akiba ili mali asili za Taifa ziwe salama kwa manufaa ya Watanzania wote.

Mhifadhi wa Pori la Akiba la Ugalla mkoani Tabora Braka Balagaye amesema programu hiyo pia itasaidia katika kukusanya ushahidi wa matukio mbali mbali ya majangili wanapokamatwa katika hifadhi za taifa, mapori ya akiba na misitu ya Serikali ambao unaweza kutumika mahakamani.

“Programu hii itawarahisishia kazi askari wanaofanya doria katika hifadhi kuweza kuifanya doria yao kimkakati na kuzaa matunda kwa kudhibiti ujangili ambao ni tatizo sugu barani Afrika katika hifadhi nyingi,"amesema Baraka.

Mkufunzi wa Programu hiyo kutoka shirika la uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori (WCS) kutoka nchini Thailand Antony Lyman amesema, programu hiyo ikitumika ipasavyo ina uwezo mkubwa wa kutokomeza kabisa matukio ya ujangili katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Maafisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za Taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini Wakifuatilia mafunzo ya naamna ya kutumia teknolojia ya Smart kwa njia ya simu na kompyuta kukabiliana na Ujangili na uharibifu wa misitu .Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka
Maafisa Wanyamapori, maliasili, ulinzi na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba ya wanyama ya serikali nchini Wakifuatilia mafunzo ya Namna ya kutumia teknolojia ya Smart kwa njia ya simu na kompyuta kukabiliana na Ujangili na uharibifu wa misitu. Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...