Na
Bashir Yakub .
1. NINI MAANA YA
KUACHISHWA KAZI KIMAKOSA.
Katika ujumla wake
kuachishwa au kufukuzwa
kazi kimakosa ni hatua
ambapo mwajiri anamwachisha
au anamfukuza kazi
mwajiriwa wake bila
kufuata utaratibu wa
sheria. Mwajiri asipofuata
sheria katika kumuondoa
mwajiriwa kazini ndipo
anapokuwa amemiwachisha kazi
kimakosa.
Na hapa haiongelewi
Sheria ya ajira
na mahusano kazini
tu inayotakiwa kuzingatiwa,
bali sheria zote
ambazo huhusika katika ajira na mikataba ikiwemo
sheria ya mikataba na
nyinginezo. Sheria yoyote
haipaswi kuvunjwa au
kukiukwa wakati mwajiriwa
anapotakiwa kuachishwa kazi.
2. AINA
MBILI ZA KUACHISHWA
KAZI KIMAKOSA.
Kuachishwa kazi kimakosa
kumegawanyika mara mbili ;
( a ) KUACHISHWA KWA
KOSA AMBALO HALIPO(WRONGFUL TERMINATION).
Hii ni pale
ambapo mwajiri anamtuhumu
mwajiriwa kwa kosa
ambalo hajatenda kabisa.
Anamtungia kosa ili
amuondoe kazini kwasababu
anazojua mwenyewe. Au
inakuwa ni kweli
mwajiriwa ametenda kosa
lakini kosa lile halina
hadhi au uzito
wa kumwondoa kazini.
Sio kila kosa
ni la kumwondoa
mtu kazini. Makosa
mengine ni ya
kuonya au kuelekeza
tu.
Kwahiyo haya
yakitokea ndipo tunaposema
kuwa mwajiriwa ameachishwa kazi
kimakosa. Kimakosa kwa
maana kwa kosa
ambalo halipo au
lipo lakini halitoshi
kumuachisha mtu kazi( not
justifiable).
( b ) KUACHISHWA KAZI
KWA KOSA AMBALO LIPO LAKINI
BILA KUFUATA UTARATIBU(UNFAIR
TERMINATION).
Hapa kosa linakuwa
ni kweli kabisa
limetendwa. Na uzito
wa kosa lenyewe
unatosha kabisa kumuachisha mwajiriwa kazi.
Tatizo linakuja kuwa
wakati wa kumuachisha
kazi kwa kosa
hilo utaratibu unakiukwa.
Kosa sawa lipo, lakini
utaratibu wa kutumia
kosa hilo kumwondoa mtu
ndio uliokiukwa.
Utaratibu ni kama
kutopewa taarifa(notice) , au
kupewa taarifa lakini
katika muda usiostahili, kutolipwa stahili, kutopewa nafasi
ya kusikilizwa, nk. Kwahiyo utaona tofauti
ya aina hizi mbili
za kuachishwa kazi
kimakosa.
Hata hivyo, pamoja
na utofauti huu bado
unachostahili baada ya
kuachishwa kazi kimakosa
ni kilekile. Aliyeachishwa
kwa kosa ambalo
halipo na aliyeachishwa
kwa kosa ambalo
lipo lakini kwa
kukiuka utaratibu wote
hustahili stahili sawa
kama tutakavyoona hapa.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...