Na Beatrice Lyimo, MAELEZO- DODOMA.
Serikali imepokea zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kwa ajili ya wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii inayojumuisha kata, vijiji na mitaa.

Zana hizo zimekabidhiwa leo mjini Dodoma kwa Kamisha wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftal Ng’ondi na Shirika la John Snow Inc(JSI) kushirikiana na MEASURE Evaluation na PACT Tanzania kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii(CHSSP) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID).

Wakati wa makabidhiano hayo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa ni muhimu kupeana taarifa katika utekelezaji wa mipango mbalimbali iliyopo ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hivyo zana hizo zitasaidia katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi.

Dkt. Naftali Ng’ondi ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi anapata huduma stahiki.

“ Zana hizi zitasadia wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii katika kuwasaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi” alisema Dkt. Ng’ondi.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi akikata utepe kuzindua zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika hafla ya makabidhiano ya zana hizo katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14, 2017  mjini Dodoma.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Dkt. Naftali Ng’ondi pamoja na wadau wakionesha zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi katika picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya Kikao cha makabidhiano ya  zana hizo kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina leo Februari 14,2017 mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...