WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wamesikitishwa na kifo cha Bw. Jerome Swai (58) aliyekuwa fundi bomba mahiri kilichotokea tarehe 26 , 2018 kwenye hospitali ya Amana baada ya kuugua kwa muda Mfupi.
Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema marehemu Swai alikuwa hakubali kushindwa kwa kuhakikisha anatatua tatizo linalohusiana na mabomba ya maji kwa wakati wote anapokuwa kazini.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Bi. Hanna Kibopile alisema marehemu ameacha pengo kubwa kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.
Naye meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, Bw. Daimon Mwakyosa alisema marehemu alikuwa akifanyakazi kwa bidii na hakukubali kushindwa.
“Marehemu alikuwa akiijua vyema kazi yake na hakukubali kushindwa nakumbuka wakati nikiwa JNIA na tukiwa tumepangwa shift (zamu) moja hakuna kilichoshindikana kwake kuhusu fani yake aliijua vyema kazi yake,” alisema Bw. Mwakosya.
Marehemu Jerome Swai
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (kulia), akimpa pole Bi. Honoratha Emmilian aliyefiwa na mume wake marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba (JNIA), alifariki tarehe 26 Februari, 2018 kwenye hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian, akitoa pole kwa Bi. Honoratha Emmilian ambaye ni mke wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa fundi bomba.
Ndugu wa marehemu Jerome Swai wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (mwenye tai) alipofika kuwafariji, ambapo marehemu alikuwa Fundi Bomba JNIA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...