Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameipongeza Kampuni ya Mzawa ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd inayojishughulisha na uchenjuaji dhahabu kwa kuthubutu kuanzisha mradi huo na aliahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kuona manufaa zaidi yakipatikana.

Alitoa pongezi hizo Machi 6, 2018 alipofanya ziara kwenye mgodi huo uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita ili kujionea shughuli ziazoendelea sambamba na kuzungumza na watendaji wake.

Biteko aliitaka kampuni hiyo kuendelea kufuata maelekezo ya Serikali ikiwemo kufuata sheria, kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali sanjari na kutunza takwimu za uendeshaji wa shughuli zao kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

Mara baada ya kupokea taarifa ya mgodi huo, Biteko aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi huo ikiwemo suala la maeneo ya uchimbaji na upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme.

“Suala la umeme nitalifikisha; tunahitaji kuona maendeleo. Tunahakikisha tunaandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji wote wa ndani na nje,”  alisema Biteko.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akikagua eneo linalojengwa mitambo ya kusagia mawe kwa ajili ya kuchenjua dhahabu katika mgodi wa Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) alipofanya ziara kwenye mradi wa kuchenjua dhahabu wa Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hussein Amar.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd Hussein Amar (kushoto) akielezea mtambo wa kuchenjulia dhahabu wakati wa ziara yake kwenye mradi wa kuchenjua dhahabu wa kampuni hiyo.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) alipofanya ziara kwenye mradi wa kuchenjua dhahabu wa Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hussein Amar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...