Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Nzega. Mkuu wa Mkoa huyo alikuwa katika ziara maalumu ya kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali katika mashamba ya wakulima wa pamba katika sehemu mbalimbali Wilayani humo.
 Mshauri wa Masuala ya Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage (mwenye shati nyeupe) akitoa kwa wakulima namna ya kuwatambua wadudu mbalimbali waharibifu wa zao la pamba katika Kijiji cha Mogwa Wilayani Nzega wakati wa  ziara maalumu ya Mkuu wa Mkoa huo kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali kuua wadudu katika mashamba ya wakulima katika sehemu mbalimbali Wilayani Nzega.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa elimu Wilayani Nzega  juu ya matumizi ya dawa ya kuua wadudu waharibifu wa pamba aina ya Dudu -All 450EC wakati wa mwendelezo wa kampeni yake ya kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya viuawadudu.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia ) na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (kushoto) wakigagua shamba la Mkulima wa pamba katika kijiji cha Chamwabo wilayani Nzega ambalo lilikuwa limeathiriwa na juu na wadudu waharibifu lakini hivi limeanza kuanza matunda mapya ya pamba(vitumba).  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...