Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga amesisitiza uwajibikaji kwa walimu ili kuleta ufanisi mkubwa katika sekta ya elimu.

Magoiga alitoa msisitizo huo wakati akikabidhi vyumba viwili vya madarasa kwa shule ya sekondari Maganzo wilayani humo vilivyokamilika vyenye thamani ya sh. milioni 19.4.Vyumba hivyo ni sehemu ya mradi uliotekelezwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na fedha ambazo zilitolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Alisema kuwa endapo walimu hao watawajibika ipasavyo wanafunzi watafanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuleta sifa nzuri katika shule pamoja na wilaya nzima kwa ujumla.Mkurugenzi Mtendaji aliongeza kwa kusema kuwa kampeni ya kufuta ziro yaani sifuri inayoendelea itaweza kupata mafanikio makubwa kama walimu watajituma katika kufundisha vizuri.

Aidha aliwataka wanafunzi kujituma na kutumia fursa ya kuwepo shuleni kwa ajili ya kusoma kwa bidii na kufaulu masomo yao hivyo kuweza kuwa watalaamu wa baadaye kwa manufaa ya jamii.

Itakumbukwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ilipata ufadhili wa fedha TEA jumla ya sh. milioni 70.5 kati y ash. milioni 141 kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa miundombinu katika shule hiyo.
Kwa kutumia fedha hizo pamoja na kushirikisha nguvu za wananchi inaendelea na ujenzi wa nyumba ya walimu sita, choo cha matundu 2 cha walimu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mwenye tai) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Maganzo wakati alipozindua vyumba vya madarasa vilivyokamilika.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akifungua moja ya vyumba vya madarasa vilivyomalika ujenzi wake wakati akivikabidhi kwenye shule ya sekondari Maganzo.
 Walimu, wajumbe wa bodi ya shule na wanafunzi (hawapo pichani) wa shule ya sekondari  Maganzo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (aliyesimama) wakati alipozungumza alipowakabidhi vyumba vya madarasa.
 Sehemu ya jengo lenye chumba cha darasa la shule ya sekondari Maganzo lililokamilika ujenzi wake na kukabidhiwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...