Na Yusuph Mussa, Korogwe.

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri,  kutafuta fedha haraka ili kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu na ofisi mbili za walimu Shule ya Msingi Msambiazi.

Amesema hayo baada ya kufanya  ziara kwenye shule hiyo leo Machi 8, 2018 na kukuta baadhi ya madarasa ya shule hiyo ni tishio kwa usalama wa wanafunzi, kwani kuta na madirisha vinataka kuanguka, hivyo kufungwa kamba ili kuzuia mabati yasiezuliwe na upepo, huku  mabati hayo yakiwa yametoboka.

Chatanda alisema wasisubiri watoto hao kupata madhara, bali wachukue hatua kwa kumaliza ujenzi wa maboma hayo ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi, Serikali na wahisani.

"Ofisa Ellimu Msingi (Elias Mavoa) naomba umfikishie salamu Mkurugenzi wa Halmashauri (Shauri). Atafute fedha za haraka tumalize madarasa haya, kwani madarasa haya ya sasa ni machakavu na mimi mwenyewe nimeyaona... haiwezekani dirisha na mbao za bati ziwe zimeshikiliwa na kamba.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda leo Machi 8, 2018 amefika Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga katika Halmashauri ya Mji Korogwe ili kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu. Pichani Chatanda akiangalia choo kipya kwenye shule hiyo, ambapo ili kukamilisha ujenzi wa choo hicho, ametoa sh. milioni 1.5 kupitia Mfuko wa Jimbo.
 Madarasa haya ndiyo yanatumika kwa sasa Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga, Halmashauri ya Mji Korogwe. Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda ambaye amefika  shuleni hapo leo Machi 8, 2018, kukagua ujenzi wa madarasa mapya matatu na ofisi mbili za walimu kwenye shule hiyo, ameitaka Halmashauri ya  Mji Korogwe kutafuta fedha kumalizia ujenzi wa madarasa hayo ili kuwaondolea adha wanafunzi wanaosoma kwenye madarasa haya, ambayo mabati yake pia yanavuja ikinyesha mvua.
Madarasa matatu na ofisi mbili za walimu Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga, Halmashauri ya Mji Korogwe. Hadi sasa ujenzi huo umegharimu sh. milioni 12 na hadi kukamilika itakuwa sh. milioni 44. 

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Mary Chatanda (kulia) akikagua majengo ya madarasa mapya matatu na ofisi mbili za walimu Shule ya Msingi Msambiazi, Kata ya Mtonga katika Halmashauri ya Mji Korogwe. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Zena Machita. (Picha na Yusuph Mussa).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...