UMOJA
wa Mataifa umeingia makubaliano ya kuimarisha upatikanaji na usambazaji
wa habari za maendeleo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
pamoja na chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO).
Makubaliano
hayo yamelenga kuimarisha upatikanaji na utoaji habari wa pamoja kuhusu
mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa serikali na malengo ya maendeleo
endelevu ya dunia.
Kwa
mujibu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro
Rodriguez makubaliano hayo yatachagiza kupatikana kwa habari kuhusiana
na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu unaokwenda sambamba na
mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa Tanzania.
Akizungumzia
malengo hayo kwa maofisa wa mawasiliano wa serikali wanaokutana mjini
Arusha kwa semina ya wiki moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya TAGCO na
Wizara ya Habari na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa, alisisitiza kuwa
malengo hayo yanahitaji kuwasilishwa kwa wananchi na pia kupigiwa
chapuo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akiwasilisha mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Ofisa Habari wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru akiuliza namna ambavyo mapambano dhidi ya rushwa yanavyoweza kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi (kulia) wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Maelezo Dk. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari nje wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.
Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano ikiwasilishwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez hayupo pichani katika mkutano huo wa 14 unaoendelea jijini Arusha.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...