WIZARA YA FEDHA NA MPANGO

UTANGULIZI

  • Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutujalia uhai na afya. Aidha, tunamshukuru kwa kutuwezesha kukutana tena hapa mjini Dodoma, kupokea mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/19, kwa mujibu wa Kanuni ya 97 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016.
  • Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutumia fursa hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kuteuliwa kwao kuwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge kuanzia sasa. Aidha, niwapongeze Wenyeviti wote na Makamu wao ambao wamechaguliwa kushika dhamana ya kuziongoza Kamati hizo. 

  • Ni matumaini yangu  kuwa Waheshimiwa Wabunge katika nafasi zenu kwenye Kamati, bila kujali itikadi, mtaisaidia kuishauri Serikali ipasavyo katika kuijenga nchi yetu kwa manufaa ya Watanzania wote.
  • Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muhtasari, matokeo ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na: nchi yetu kuendelea kuwa na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi ya wastani wa asilimia 7.0 kwa mwaka ambayo inatafsiri Pato la wastani la kila mtu kuwa shilingi 2,131,299 mwaka 2016 kutoka shilingi 1,918,930.9 mwaka 2015; kupungua kwa mfumuko wa bei kufikia asilimia 4.1 Februari 2018; kuongezeka kwa mapato ya ndani kufikia wastani wa shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi kutoka wastani wa shilingi bilioni 850; 

  • kuimarika kwa utoaji wa huduma za jamii hususan elimu msingi bila ada, kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma kwa ngazi zote ikiwemo huduma za matibabu ya kibingwa, kuimarika usambazaji wa maji mijini (kufikia wastani wa asilimia 78) na vijijini (wastani wa asilimi 55.5), umeme mijini na vijijini kufikia wastani wa uunganishaji wa asilimia 67.5 kitaifa na kuweka mazingira wezeshi kwa ujenzi wa viwanda ambapo viwanda vipya 3,306 vimejengwa.
  •  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor  Mpango  (Mb)   akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma.
     Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma.
     Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 Bungeni Dodoma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...