Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kila chombo kinapaswa kufanya kazi zake kwa kuheshimiana na haipendezi kila mara zitolewe amri ambazo hazitekelezwi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameyasema hayo leo Aprili 11 mwaka wakati kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkaboli mmiliki wa IPTL Harbinder Sethi na mwenzake, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutekeleza amri aliyoitoa ya kumpeleka mshtakiwa Sethi kutibiwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili.

"Ninaamini, kila chombo kinapaswa kufanya kazi zake kwa kuheshimiana, haipendezi kila wakati tutoe amri ambazo hazitekelezwi, hivyo naamuru apelekwe hospital kinyume na hapo nitatoa amri nyingine kwa mujibu wa sheria,"amesema Hakimu  Shaidi.

Mapema, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mahakani hapo upelelezi wa kesi hiyo bado hujakamilika, pia wameshindwa kumpeleka Sethi hospital kwa sababu Sethi alihamishwa gereza kutoka Segerea kwenda Ukonga, pia alidai mshtakiwa aliomba daktari wake kutoka Afrika Kusini awepo wakati akipatiwa matibabu.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula alipinga vikali Hoja hizo na kudai kuwa hazina msingi kwa sababu Sethi hakuwahi kuzungumzia suala la daktari na kuongeza, kuwa katika gereza la Ukonga Sethi haruhusiwi kuonana na mtu yoyote hata mke wake wa ndoa.

Kutokana hoja hizo,  Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 25 mwaka 2018.

Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya dola za Marekani USD 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...