Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MUGIZAJI wa filamu za kibongo nchini Salim  Ahmed a.k.a Gabo, ametangazwa kuwa balozi wa simu mpya ya mkononi kutoka Kampuni ya Tecno Tanzania iliyopewa jina la Tecno Pop 1 ambayo itauzwa kwenye maduka yote ya Vodashop nchini.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa  kumtangaza Gabo kuwa balozi wa simu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno,Anuj Khosla amesem wameamua kuileta simu hiyo ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha  chini kumiliki simu janja .

"Tuna furaha kubwa kuwatangazia uwepo wa simu hii ambayo mtu akinunua atapata na GB 10 kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ili kuperuzi mtandao na kujielimisha kupitia simu hii janja ambayo ina uwezo mkubwa,"amesema Khosla

Kwa upande wake Gabo amesema anaishukuru Tecno kwa kumpa nafasi hiyo ya kufungua njia kuwa balozi kwani ndio ubalozi wa kwanza kuupata tangu aanze kujulikana katika tasnia ya filamu.

"Naamini huu ndio mwanzo wa mimi kuendelea kufanya kazi na kampuni kubwa baada ya hii kampuni ya simu kuniona Gabo na kunifanya kuwa balozi wa kutangaza bidhaa zao.Ni jambo jema ambalo kila msanii anatamani kulifikia ukiacha mafanikio ya sanaa ya kawaida,"amesema Gabo.


Amesema kwa sasa yeye kama msanii mkubwa anatumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa mashabiki na kuwataka watumie simu hizo ambazo zina ubora na bei nafuu mpaka kwa watanzania wa kawaida.
 Mkuu wa kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno, Anuj Khosla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Simu mpya ya Tecno POP 1 itakayotolewa na GB 10 za Vodacom   leo Jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa Filamu wa nchini, Salim  Ahmed "Gabo", akionyesha simu aina ya Tecno POP inayotolewa na GB 10 Za Vodacom. kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi  ya rejareja ya simu kutoka Vodacom, Brigita Stephene.
Msanii wa Filamu wa nchini Salim  Ahmed "Gabo" akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Vodacom na Tecno Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...