Mhe.
Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano jana jioni
alikuwa ni miongoni mwa Jopo lililojadili kuhusu sera za kumwinua
mwanamke kiuchumi wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wanawake linalofanyika
kama sehemu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola
(CHOGM) unaoendelea hapa London.
Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe. Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ya wanawake.
Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe. Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ya wanawake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimia na Waziri Mkuu wa Malta Mhe.
Dkt. Joseph Muscat
mara baada ya mkutano wa Jukwaa la Wanawake kumalizika jijini London, Uingereza.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la Wanawake ikiwa Sehemu ya
mkutano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini London, Uingereza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...