-Wekeni
hata kwenye nyumba za nyasi
Na Tiganya Vincent
SERIKALI imesema ni marufuku kwa Wakandarasi na Wataalamu kuruka nyumba wakati wa uunganishaji wa umeme kwa wananchi kupitia Mradi kabambe wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatuunatekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Urambo na Kaliua na Waziri wa Dkt. Medard Kalemani wakati alipokuwa akigaua utekelezaji wa zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo hayo.
Alisema ni marufuku kuruka nyumba hata kama ni nyasi kama mwananchi anataka umeme na amelipa shilingi 27,000 za kuunganishiwa umeme.
Kalemani alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafika katika vijiji na vitongoji vyote na kwa wananchi wote bila kubagua.
“Nawaagiza Wakandarasi na Wataalamu wote hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba kwa sababu ya kuwa imeezekwa kwa nyasi…umeme ni nyumba kwa nyuma , kaya kwa kaya.., hata kama mtu hajakamisha nyumba yake kama kuna mti karibu na nyumba yake wekeeni hata hapo ili iwe rahisi kuingiza umeme atakapokuwa amekamisha nyumba yake” alisisitiza Waziri huyo.
Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo
Magreth Sitta na viongozi wengine wakikata utepe wa uzinduzi wa uwashaji
wa umeme wa REA katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele
jana.
Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani akibonyesha kitufe kuwasha umeme katika
Kijiji cha Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele baada ya kukamilika kwa
mradi wa uwekaji wa miundombinu katika eneo hilo.
Waziri
wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo
Magreth Sitta(kushoto) na wananchi wa kiijiji cha Jionee Mwenyewe kata
ya Songambele wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme
katika eneo hilo jana.
Waziri
wa Nishati Medard Kalemani akimpongeza Diwani wa Kata ya Vumilia
kupitia ACT Wazalendo Kassim Shushu (kushoto) baada ya kumkabidhi eneo
la shamba lake linalokadiriwa kuwa ekari moja kwa ajili ya ujenzi wa
Kituo cha Kupozea umeme. Picha na Tiganya Vincent
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...