Picha na Habari za Freddy Macha
Ulikuwa mkutano mfupi uliokusudia kutoa shukrani
kwa wafadhili na Watanzania London wanaosaidia nyumbani. Fadhila hupitia
Jumuiya ya Waingereza na Watanzania
(BTS) na kitengo chake cha TDT = shirika la Mfuko wa Maendeleo Tanzania.
BTS ilianzishwa mwaka 1975, na mlezi
wake sasa hivi ni Rais mstaafu Ali Mwinyi.
BTS ilimkaribisha Makamu wa Rais Mheshimiwa Suluhu
Samia, aliyekuja London wiki hii kudhuruia mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola.
Kawaida viongozi hutegemewa hotuba ndefu zenye maelezo yanayochosha
masikio.
Mhe Suluhu alitua chuo kikuu cha lugha za Afrika
na Mashariki ya Kati (SOAS) akasalimiana
na kupeana mikono na wananchi wa pande zote mbili. Hiyo tu ilitosha kuonesha
imani yake kwa wananchi wachapa kazi wa pande hizi mbili.
Makamu wa Rais Mhe Suluhu Samia akizungumza na Dk Mohammed Hamza, kiongozi
wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Uingereza
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dk Asha Rose Migiro akiwa na Kaimu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe Marc Thayre
Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Uingereza na Tanzania (BTS) Dk Andrew Coulson
aliyefungua na kufunga kikao cha Brunei Gallery, SOAS.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo. Kutoka
kushoto ni Kiondo Wilkins, Dk Alex
Paurine, Simon Mzuwanda na Joe Warioba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...