Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
BARBARA Bush mke wa Rais wa 41 wa Marekani George Herbert Bush na mama wa George W. Bush Rais wa 43 wa Marekani amefariki dunia jana April 17 akiwa na miaka 92, ofisi ya ya George H. W yathibitisha.
Bi Barbara alikuwa mhimili wa siasa kwa mumewe aliye na miaka 93 sasa pamoja na mwanaye George W.Bush aliyehudumu kama Rais wa Marekani kwa miaka minne kuanzia mwaka 2000, chanzo cha kifo chake kinaelezwa ni maradhi yaliyosababishwa na umri hali iliyompelekea kudhoofu.
Bi Barbara alizaliwa Manhattam na kuhitimu masomo yake Ashley Hall huko Carolina Kusini, alikutana na George Herbert Bush akiwa na miaka 16 na kufanikiwa kupata watoto sita wakiwamo George W. Bush Rais wa 43 wa Marekani na Jeb Bush Gavana wa 43 wa Florida. mwezi januari mwaka huu walitimiza miaka 73 ya ndoa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...