Sehemu ya Magari pamoja na Watembea kwa miguu wakipita katika eneo la Jangwani, jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kufunguliwa rasmi jioni ya leo. Eneo hilo lilifungwa kwa muda kutokana na kufurika maji yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika meneo mengi hapa nchini.
Mabasi ya Mwendo kasi yakipita katika njia yake baada ya kufunguliwa rasmi barabara ya Morogoro eneo la Jangwani, ambalo lilifungwa kwa muda kutokana na kufurika maji yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika meneo mengi hapa nchini.
Sasa mabo yamerejea kama ilivyokuwa awali.
Katapila likiendelea na zoezi la kusukuma maji ili kufanikisha kupatikana kwa njia.
Mwendesha baiskeli akikatika eneo la Jangwani kwa mtindo wa miguu juu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...