Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Mb.) akihutubia kwenye Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani, unaowakutanisha wadau mbalimbali wanao simamia na kutengeneza vifaa na miundombinu mbalimbali ya Tehama. Mkutano huo unatarajia kuangalia namna mbalimbali za kupambana na matumizi ya Tehama yanayochafua mazingira; umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwemo Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dkt. Sira Ubwa (Mb.), Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi, Mkurugenzi wa ITU (International Telecomunication Union), Dkt. Chaesub Lee, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Kilaba. Mkutono huo unafanyika katika Hoteli ya Sea Clif Mangapwani, Zanzibar kuanzia tarehe 9-12, Aprili 2018. 
Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo visiwani Zanzibar na kuelezea faida ya mkutano kufanyikia Unguja. Alisema kwa mazingira ya sasa, changamoto iliyopo mbele yetu ni kushirikiana kwa pamoja ili kuziepusha nchi zetu na uharibifu utokanao na matumizi ya vifaa chakavu vya kielektroniki. Mhe. Dkt. Sira alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa mjadala muhimu utakaoendelea wa utunzaji wa mazingira na kuwasihi wasiache kutembelea vivutio vya asilia vilivyopo visiwani humo. 
Mkurugenzi wa International Telecommunication Union (ITU) Dkt. Lee akizungumza kuhusu mjadala na maazimio ya mkutano huo muhimu wa kimataifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Wiki ya Kijani. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...