Na Mwandishi Wetu
Zabron Mbwaga ambaye ni Mzalishaji mbegu, aliyepo Viwanja vya NaneNane, Njiro mkoani Arusha ametwaa tuzo ya mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali ya Citi Foundation. Tuzo hiyo inaambatana na fedha taslimu dola za Marekani 7,500.
Mbwaga ambaye aliwezeshwa upanuzi wa shughuli zake kwa mikopo kutoka BRAC Tanzania, alianza kazi zake akiwa na mtaji wa shilingi milioni 2 kabla ya kuongezewa nguvu na BRAC.
Tuzo hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki zilitolewa kwa wajasiriamali 16 na ofisa mikopo mmoja.
Mshindi wa pili ni Anney Sekulasa akiondoka na dola za Marekani 6000 huku mshindi wa tatu ni Lydia Majoro ambaye aliondoka na dola za Marekani 4000. Nafasi ya mjasiriamali mlemavu ilitwaliwa na Aneth Geraw aliyepata dola za Marekani 2000.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu
(kulia) akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa tuzo za Ujasiriamali za
Citi Foundation, Lydia Majoro wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini
Dar es Salaam.
Mjasiriamali
mlemavu aliyefanya vyema Aneth Geraw ambaye aliondoka na kitita cha
dola za Marekani 2000 wakati hafla ya kukabidhi tuzo za ujasiriamali za
Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa
mshindi wa pili wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Anney
Sekulasa (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia tukio hilo katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) na Mkurungenzi wa Fedha
na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati)
kwa pamoja wakikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu
Microfinance, Attemius Millinga (kushoto) ambapo taasisi yake imekuwa na
ubunifu mkubwa wa bidhaa zake sambamba na mifumo ya kutolea huduma na
methodolojia wakati wa hafla fupi ya tuzo za ujasiriamali za Citi
Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanamke
aliyefanya vyema kwenye ujasiriamali mdogo, Lucy Kiongosi akipozi baada
ya kupokea cheti kilichoambatana na dola za Marekani 2000 wakati wa
hafla ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika mwishoni
wa wiki jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila na kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...