Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

KIKOSI cha Simba kimeendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya hapo kesho.

Mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa utawakutanisha timu hizo huku Mbeya City akitaka kujinasua kutoka katika hatari ya kunusa kushuka daraja huku Simba wakitaka kuendelea kukalia kiti cha uongozi wa ligi.

Kikosi hicho cha Simba kinajifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo jijini Dar es Salaam leo asubuhi na jioni.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba iliwakosa wachezaji Juuko Murushid, James Kotei na Erasto Nyoni ambao walikuwa wanatumikia adhabu ya kadi 3 za njano kwa kila mmoja.

Tayari wachezaji hao wameshamaliza adhabu hiyo na kesho wanatarajia kuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi  Simba.

Kocha Msaidizi wa Simba Masoud Djuma ameonekana hana wasiwasi na kikosi chake kuelekea mchezo huo wa kesho ambapo anaamini ushindi ndiyo jambo la msingi ili kupata ubingwa wa msimu huu.

Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 52 wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga wenye alama 46 ambapo wanacheza leo dhidi ya Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...