Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akiwammiliki wa leseni za vitalu vya gesi na mafuta
nchini kwa kushirikiana na mkandarasi, kampuni ya Dodsal wanaendelea kufanya utafiti (ukusanyaji
wa takwimu za mitetemo “2D seismic data” utafiti unahusisha eneo lenye urefu wa takribani km
1287) zaidi wa gesiasilia katika Kitalu cha Ruvu kilichopo Mkoa wa Pwani na baadhi ya maeneo ya
Dar es salaam kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gesi asilia au mafuta ya kutosha
itakayojenga uchum iimara wa viwanda.
Akielezea umuhimu wa utafiti huo, Simon Kimario ambaye ni Mjiofizikia kutoka TPDC
amesema kuwa lengo kuu la utafiti huo nimuendelezo wa utafiti wa mafuta na gesi unaofanywa na
mwekezaji Dodsal Hydrocarbons akishirikiana na TPDC katika kitalu cha Ruvu ilikuwezesha kugundua
gesi asilia nyingi zaidi na pengine mafuta ilikuhakikisha Taifa linakuwa na chanzo imara cha nishati
ambacho kitalisaidia taifa katika kujenga uchumi wa viwanda.
Ramani inayoonyesha kitalu cha utafiti cha Ruvu
“Tayari hatua kadhaa zimeishafanyika kama vile; uandaaji wa ramani ya kiutafiti ambayo kazi yake
nikuonyesha eneo la kitalu na maeneo muhimu ya kufanyia utafiti, ambapo kunapelekea kwenye
hatua nyingine ya kwenda kwenye eneo halisi na kubaini mistaria ambayo taarifa za mitetemo
zitachukuliwa, hatua ambayo itanguliwa na zoezi la kupata vibali na kuelimisha wananchi kuhusu
namna zoezi zima na ushirikishwaji wa wananchi utakavyofanyika.”
Akiogelea hatua zinazoendelea sasa hivi ndugu kimario anaeleza kuwa shughuli zinazoendelea katika
maeneo tofauti tofauti kwa sasa ni pamoja na usafishaji njia au mistari, kuchimba mashimo ya kina
kifupi mita 7, 10 au 15 kutegemea na jiolojia ya eneo kwa ajili ya kuweka baruti (vyanzo vya
mitetemo ) pamoja na kuweka mitambo maalum ya kuchukulia taarifa za mitetemo(seismic data).
Mtambo wa kuchoronga mashimo ya kuwekea baruti ukiwa kazini. Mtambo huu huchimba mashimo
yenye urefu tofauti kati ya mita 7 hadi 15, kwaajili ya kufukia baruti ambazo zinapolipuliwa ndipo
taarifa za miamba chini hupatikana baadae kuchakatwa na kutafsiriwa kitaalam ilikujua sehemu ya
kuchimba kisima cha utafiti.
Aidha anaeleza kuwa, “Yapo maeneo mengine ambayo yamefikia kwenye hatua ya kubainisha
maeneo maalum yatakayowekewa baruti pamoja na vifaa vya kunakili au kunasa taarifa za
mitetemo, yapo maeneo ambayo tayari zoezi hili limeshafanyika na tayari hatua ya kulipua baruti na
kunakili taarifa za mitetemo limekwishaanza kufanyika”.
Simon amethibitisha kuwa hadi sasa takribani mashimo yaliyopo kwenye misatri yenye urefu
wa km 311 yameishasimikwa au kujazwa na baruti na mistari ya kijiofizikia yenye urefu wa Kilomita
116.9 kati ya 1287 imeshachukuliwa taarifa za kijiofizikia na kuendelea kufanyiwa uchambuzi wa
awali.
Mmoja wa wataalam wa milipuko akipima urefu wa shimo kama limekidhi mahitaji ya kitaalam kabla ya kusimika/kujaza baruti ndani ya shimo.
Aidha akiongolea suala la vibali na fidia kwa wananchi ambao mazao yao yameathirika na
yatakayoathirika na zoezi la uchukuaji wa taarifa za mitetemo, Mohamed Ally ambaye ni
Msimamzi wa Vibali kutoka kampuni ya Envision Consulting Ltd ameeleza kuwa kumekuwa na
ushirikiano mkubwa sana kutoka TPDC haswa panapohitajika vibali kutoka katika mamlaka
mbalimbali za serikali na hivyo kumefanya kazi yao kuwa rahisi na yenye mafanikio.
Akiongolea suala la fidia, Mohamed anabainisha kuwa “pamoja na kuwa na mtathamini
wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kushirikiana na viongozi kutoka ofisi za Kata, Wilaya, Mikoa
pamoja Mthamini Mkuu wa wa Serikali na hivyo kufanya zoezi zima la uthamini na ulipaji fidia
kufanyika kwa mafanikio makubwa na kupunguza migogoro na wananchi”.
Moja ya baruti zinazofukiwa chini ikiwa kwenye maandalizi ya kufukiwa kwenye shimo maalum kwa ajili ya kulipuliwa.
Pamoja na utafiti unaofanyika katika kitalu cha Ruvu, TPDC linaendelea na maandalizi ya utafiti
katika maeneo mbalimbali nchini kama vile vitalu vya; Eyasi-Wemberi, Songo Songo Magharibi,
Mnazi Bay kaskazini pamona na Vitalu vya 41B/41C.
Moja ya kitafaa maalumu (AVO) ya kunakili taarifa za mitetemo za kijiofizikia kikiwa kimesimikwa
ardhini tayari kusubiri mitego ya baruti kulipuliwa ili kupata taarifa za mitetemo. Mtambo huu
hutumika ili kupata taarifa za mitetemo zenye taswira ya pande mbili “2D”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...