Watanzania
wamehimizwa kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kwa ajiri ya kuibua
fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuacha tabia ya kutumia vitabu kama sehemu salama ya kuhifadhia fedha , kama ilivyo kwa baadhi ya watu maeneo ya vijijin na mjini huku waandishi wa vitabu wakitakiwa kuendelea kuandika vitabu kwa lengo la kujenga Taifa lenye wasomi.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof, Ganka Nyamusogoro
wakati wa uzinduzi wa siku ya kusoma vitabu duniani katika chuo kikuu
cha Mzumbe mkoani Morogoro, ambapo amesema jamii nyingi za kitanzania
zimejenga tabia ya kutosoma vitabu kama njia ya kuibua fursa na
kuongeza maarifa baadala yake wanatumia vitabu kama sehemu ya
kuhifadhia fedha jambo ambalo ni kinyume na na malengo ya waandishi wa
vitabu.
Makamu mkuu
wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka
Nyamusogoro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya kusoma vitabu
Duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
Makamu mkuu
wa chuo kikuu cha Mzumbe prof,Ganka
Nyamusogoro akikagua moja ya vitabu vilivyooneshwa na chuo cha mzumbe wakati
wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu Duniani,ambapo chuo cha mzumbe kimetoa
nafasi kwa watu mbalimbali kusoma vitabu katika eneo hilo ambalo lipo maalumu
kwa siku tatu chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo ya kusoma vitabu.
Wanafunzi wa
chuo kikuu cha mzumbe mkoani Morogoro na
shule ya sekondari Mzumbe wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu
duniani ambaye pia ni makamu mkuu wa chuo hicho Prof, Ganka Nyamusongoro hayupo
pichani.
Diwani wa kata
ya Mzumbe mkoani Morogoro Recho Kungi wa kwanza kushoto akisisitizia wanafunzi juu ya umuhimu wa kusoma vitabu katika maadhimisho
ya siku ya kusoma vitabu duniani yaliyo fanyika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani
Morogoro.
Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka Nyamusogoro ambaye pia ni Mgeni
rasimi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani chuo kikuu
Mzumbe Mkoani Morogoro akisoma vitabu vya tafiti vilivyofanywa na
wanazuoni wa chuo kikuu cha mzumbe mara baada ya kuzindua hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...