Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirika la Ndege linaloongoza Tanzania, Precision Air, limeshiriki katika jitihada za kuhifadhi mazingira katika maeneo ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Katika kutimiza zoezi hilo, wafanyakazi wa shirika hilo wakishirikiana na wanakijiji wa kijiji cha Ngarony pamoja na wafanyakazi wa wilaya ya siha wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Siha Valerian Juwal wamefanikisha upandwaji wa miti 1000 (elfu moja) katika eneo linalotenganisha kijiji cha Ngarony na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Akizungumzia tukio hilo Meneja Masoko na Mawasiliano wa Precision Air Hillary Mremi amesema, Precision Air inatambua inawajibu wa kutunza mlima Kilimanjaro kwani mlima huo una mchango wa moja kwa moja katika shughulli za shirika hilo.
“Mlima Kilimanjaro unatutunza vyema sisi kama shirika na kama taifa kupitia utalii, hivyo sote tunawajibu wa kuutunza mlima huu na mazingira kwa ujumla wake.” Mremi alisema.
Precision Air imekua ikifanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka ishirini na nne (24) na kama mdau mmojawapo wa utalii, limefanya zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuhakikisha jamii inayo uzunguka mlima inaendelea kufaidika na uwepo wa mlima, ambao ni moja ya kivutio muhimu cha utalii nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Siha Valerian Juwal amesema kuwa Shirika la Ndege la Precision Air limeonyesha mfano wa kuigwa na wadau wengine wa mazingira na utalii.
Na ameongeza kuwa ni wakati sasa wa kuchukua hatua madhubuti kulinda mazingira yetu ili vizazi vijavyo viweze kufaidika na uzuri wa nchi yetu wa vivutio kama mlima Kilimanjaro na vingine.
Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko amesema kuwa Precision Air wamefanya jambo zuri katika tasma nzima ua uhifadhi mazingira pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali na wananchi kwenye uhifadhi wa msitu huo.
Wafanyakazi wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza zoezi la kupanda miti 1000 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Shirika la ndege la Precision Air, Hillary
Mremi pamoja na Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko
wakiotesha mti kandokando ya mto uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Msitu wa Mlima Kilimanjaro
Wanakijiji wa Kijiji cha Ngarony kata ya Siha wakiotesha miti kwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Precision Air katika Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro (KINAPA) katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu.
Wafanyakazi wa ndege wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja na wanakijiji mara baada ya kutoka kupanda miti 1000 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...