Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii, Ruvuma

SERIKALI ya Mkoa wa Ruvuma, kupitia Jeshi la Polisi limeendesha mafunzo rasmi kwa madereva wa Malori yanayofanya safari za masafa marefu na mafupi kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani.
Miongoni mwa madereva waliopewa mafunzo ni madereva wa magari makubwa wanaobeba makaa ya mawe kutoka mkoani Ruvuma kwenda mikoa mingine pamoja na nchi jirani.
Taarifa kwa vyombo vya habari imesema kuwa katika mafunzo hayo madereva wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani kwa lengo la kujikinga na ajali ambazo husababisha vifo na majeruhi.
Semina hiyo imetolewa na Jeshi la Polisi mkoa katika eneo la Kitai wilayani Mbinga ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkoa wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ya kuwataka wadau kuungana katika kuzuia ajali za barabarani.
 Kauli mbiu ya mafunzo hayo inasema: "Ruvuma bila ajali inawezekana, Usalama unaanza na mimi".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...