Na George Binagi, Morogoro
 Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko leo amekamata madini ya vito aina Rhodilite (BOFYA HAPA kuyajua)  yanayokadiriwa kuwa tani saba katika nyumba ya mchimbaji na mfanyabiashara mmoja wa madini iliyopo Kata ya Magoweko wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Aliyekamatwa na madini hayo ambayo bado thamani yake haijafahamika ni Bw.James Mnene ambaye ni mchimbaji na mmiliki wa kampuni ya madini ya JJ.Mnene & Partiners inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito katika machimbo ya Rubeho wilayani Gairo.
Mfanyabishara huyo amejitetea kwamba alikuwa ametunza madini hayo nyumbani kwake huku akitafuta soko na kuomba asamehewe kwani yuko tayari kufuata taratibu za biashara ya madini.
Nyumba ya mfanyabiashara aliyekutwa amehifadhi madini ya vito wilayani Gairo 
Madini hayo yakiwa nyumbani kwa mfanyabishara huyo
Mashine iliyokutwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambayo ilikuwa ikitumika kusagia mawe ya madini hayo
Naibu Waziri Biteko (kushoto) akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa mfanyabishara huyo (katikati). Mfanyabiashara huyo ametiwa nguvuni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo anatuhumiwa kukweka kulipa mapato ya serikali kwani tangu mwaka 2013 amelipa shilingi laki nne

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...