Na Hadija Seif, Globu ya jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na uharifu uporaji,ukabaji pamoja na unyang'anyi .
Akizungumza leo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Liberatus Sabas amesema jana saa 03:30 raia wema walitoa taarifa kuwa kuna mtu mmoja anamiliki silaha ambapo ufuatiliaji ulifanyika haraka na ndipo alikamatwa mtuhumiwa huyo.
Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Temeke kisuma Bar maarufu Kama Sugar Ray'' akiwa na bastola iliyotengenezwa Jamhuri ya CZECH yenye namba ya usajili A.368021. Kamanda Sabas amesema jina la mtuhumiwa huyo limehifadhiwa na kwa sababu za kiupelelezi.
Aidha amesema watuhumiwa wengine wamekamatwa maeneo ya Kariakoo akiwewemi Amin Kimaro( 55)mkazi wa Manzese na wenzake watatu.
Amefafanua sababu za kukamatwa kwa kosa la kughushi hundi za benki mbalimbali jijini na kuziweka hundi hizo katika akaunti ya benki ili kufanikiwa kuiba fedha walizokusudia.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...