Na Boazi Mazigo, Afisa Habari Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameendelea kufuatilia hatua za utekelezaji wa Miradi mbalimbali Mkoani Geita kwa kufanya ziara na kuona miradi inayotekelezwa kwa fedha za Huduma kwa Jamii (CSR) kutoka Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM).
Ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mzunguko wa Kisasa (Round About) inayojengwa Halmashauri ya Mji wa Geita. Amewapongeza mafundi, akashauri ujenzi uendelee siku zote ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.
Mhandisi Gabriel amesema na wasimamizi wa mradi kwa kusema, ‘zingatieni thamani ya fedha (Value for Money) na ubora, lakini pia ikibidi mnara unaojengwa ukamilike kabla ya mwaka kuisha kwa kuwa sisi waandisi tukiwa na sikikuu nchi haitajengwa’. Pia amesifu usanifu wa mchoro wa Mnara utakao kaa katikati ya Round About hiyo ukiwa na uwakilishi wa vitu mbalimbali mfano alama ya Mwenge wa Uhuru (uwakilishi wa taifa letu), Matofali ya Dhahabu (alama ya utajiri wa madini) lakini pia itakuwepo saa ambayo inaonyesha kiwango cha joto.
Kwa upande mwingine, Mhandisi Gabriel ameushukuru uongozi wa Mgodi wa GGM baada ya kutembelea na kuona jumla ya mifuko ya saruji 2,136 iliyopelekwa Halmashauri ya Mji Geita katika utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya  Elimu na Afya kisha kujionea hatua ya uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kisasa inayoanza kujengwa eneo la Magogo lililotengwa kwa ajili ya Shule. Mkuu wa Mkoa kwa mara nyingine akasema; angependa kuona ujenzi wa Shule hiyo inaanza mara moja, maboma yakamilike ndani ya miezi mwili na nusu, kisha ukamilishaji ufuatie na yeye atashiriki kwa kuwa msimamizi wa shughuli ya ujenzi akizingatia thamani ya fedha hivyo aliwataka wananchi kuanza usafi mara moja kwani tayari baadhi ya vifaa vya ujenzi kwa nguvu za wananchi vipo kwenye eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa alisisitiza kwa kusema, “kwa kuwa tunatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya  Chama Tawala CCM, na kwa kasi ninayoiona, tukikaa vizuri kufikia mwakani, Zahanati kila Kijiji tunamaliza kabla ya Uchaguzi Mdogo wa mwaka 2019 kwani maboma yakikamilika tutakuwa juu ya asilimia 80 upande wa Sekta ya Afya. Hata kwa upande wa elimu, maendeleo siyo mabaya” aliongeza.
Alipofika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mhandisi Gabriel aliona mifuko 680 ya saruji na kupokea taarifa iliyoeleza kuwa bado mifuko 1,459 haijawasilishwa na kwamba kufikia wiki ijayo itakuwa imefika. Lakini pia aliagiza ujenzi uanze wiki inayofuata kwakuwa anapanga kutembelea utekelezaje wake.
Miongoni mwa alioambatana nao katika ziara hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Herman C. Kapufi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita pamoja na wawakilishi wa Mgodi wa Dhahabu Geita GGM
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akishukuru uongozi wa Mgodi wa GGM baada ya kutembelea na kuona jumla ya mifuko ya saruji 2,136 iliyopelekwa Halmashauri ya Mji Geita katika utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya  Elimu na Afya kisha kujionea hatua ya uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kisasa inayoanza kujengwa eneo la Magogo lililotengwa kwa ajili ya Shule.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akitembezwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akikagua maendeleo ya ujenzi wa mzunguko wa kisasa (Round About) inayojengwa Halmashauri ya Mji wa Geita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...