Mkurugenzi
Mkuu wa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF William Erio
ametembelea daraja la Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande
cha barabara ya lami yenye urefu wa Kilomita mbili inayo unganisha
daraja la Nyerere na barabara ya Feri - Kibada iliyopo Kigamboni jijini
Dar es Salaam.
Akikagua barabara hiyo mwishoni mwa wiki, William Erio amemtaka Mkandarasi CRJE kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa haraka na kuhakikisha gharama ya ujenzi hazizidi kiasi cha gharama kilicho kubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi kati ya NSSF na Mkandarasi huyo.
Kwa upande wa Mkandarasi amepokea maelezo ya Mkurugenzi Mkuu na kuahidi kutekeleza ujenzi huo. Pamoja na kuahidi utekelezaji, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda kutokakana na changamoto za kupatikana kwa malighafi ya udongo hasa ile ya G15.
Gharama ya mradi huu ni Tsh 21.3 billioni ambao unahusisha ujenzi wa barabara yenye njia sita, tatu kila upande zenye urefu wa kilomita mbili kutoka mwisho wa daraja hadi kwenye makutano ya barabara ya Fery - Kibada.
Pia, ujenzi unajumuisha mzunguko wenye mita za mraba 5,762, mifereji ya maji taka na yale ya mvua, kingo za katikati ya barabara "new jersey barriers", kalavati nne za umbo la boksi na moja ya ya umbo la bomba.
Sehemu ya kipande cha barabara unganishi kutoka mwisho wa daraja upande wa Kigamboni kuelekea barabara ya Ferry - Kibada.
Kaimu
Meneja wa Miradi NSSF Abdon Mhando (wa pili kushoto), akitoa maelezo ya
utekelezaji wa mradi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio (wa
kwanza kushoto), wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na
Miradi wa NSSF Bw. Gabriel Silayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...