*Sugu asema msiba upo nyumbani kwake Salasala Dar es salaam,
mwili kusafirishwa Mbeya baada ya taratibu zitakapokamilika
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MAMA mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' kupitia Chadema, amefariki dunia leo akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).Mama wa Sugu alikuwa amelazwa katika hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa msiba huo.
Kwa upande wake Sugu ameiambia Michuzi Blog kwa njia ya simu kwamba msiba wa mama yake npendwa upo nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam."Kama ambavyo mmesikia mama amefariki leo tena mchana huu, hivyo nachoweza kusema mama hatunaye na msiba upo nyumbani Salasala.
" Hata hivyo tutasafirisha msiba kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa mama. Tutatoa ratiba rasmi hapo baadae. Ila itoshe kusema msiba upo Salasala wakati tunaendelea na taratibu nyingine,"amesema Sugu.
Michuzi Media Group(MMG) inaungana na Watanzania wengine kutoa pole kwa familia ya Sugu, ndugu, jamaa na marafiki.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
===== ======= ======== ========

Mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi almaarufu kama SUGU akiwa na Mama yake MzazI enzi za uhai wake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...