Na Judith Mhina-MAELEZO
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter, amesema hajawahi kuona amani anayoiona hapa Tanzania.

Amesema maneno hayo wakati wa mahojiano maalum na Idara ya Habari MAELEZO mapema wiki hii katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Mheshimiwa Balozi Waechter amesema “Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni kiongozi ambaye hatasahaulika kwa kuwa amani aliyojenga Tanzania ni ya pekee haipatikani mahali popote duniani”. 

Kwa kutambua hilo Balozi amesema kuwa Ujerumani imeona umuhimu wa Baba wa Taifa la Tanzania kama mfano wa kuigwa duniani kwa kujenga amani na usalama wa binadamu. Ambapo watu wa dini tofauti, makabila tofauti na asili tofauti wanakaa pamoja na kushirikiana kujenga nchi. Huu ni urithi na funzo kubwa kwetu ambapo Julius Nyerere ametuachia.

Kutokana na amani na usalama wa binadamu alioujenga, Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani imejifunza jambo kubwa sana kutoka kwa Mwalimu Nyerere na kuona ni busara kufadhili jengo la Makao Makuu la Umoja wa Afrika pale Adiss Ababa Ethiopia. Linaloitwa The Julius Nyerere Peace and Security Building.

“Jengo lile ni kielelezo tosha kuwa vizazi na vizazi vitakavyofika pale Addiss Ababa Ethiopia watatambua uwepo wa Mwalimu Nyerere duniani na pia, anakumbukwa kwa Amani na Utulivu alioujenga akiwa hapa duniani na kamwe hatasahaulika” Amesisitiza Balozi Waechter.

Balozi Waechter amesema kuwa kwa muda nilioishi hapa Tanzania, tangu 2016 ninashangazwa kuambiwa watanzania ambao walio wengi ni Wakristu na Waislamu wanaoishi pamoja na kushirikiana kwa upendo na mambo yanaendelea kama kawaida. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...