BENKI ya TIB corporate imeshiriki katika maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.
Maonyesho hayo yalizinduliwa jana Oktoba 23 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuudhuriwa pia na viongozi wengine pamoja na waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashra Dkt.Stella Manyanya.
Kauli Mbiu ya maonyesho haya ni “Pamoja Tujenge Viwanda kufikia Uchumi wa Kati”
Benki ya TIB Corporate ikiwa ni mdau wa karibu wa maendeleo mbali mbali tayari imeshatoa mkopo wa shilini bilioni 1.5 kwa wilaya ya Bariada kuwezesha mradi wa upimaji wa Viwanja vya mipango miji mkoani humo.
Kwa sasa Benki ya TIB Corporate inashirikiana na SIDO ili kuvumbua fursa ambazo benki itaweza kuwapatia wajasiriamali wa viwanda vidogo na kukuza biashara zao
Benki ya Corporate ni Benki ya biashara na inatoa huduma zote za kibenki kwa watu binafsi, Makampuni Binafsi, taasisi za serikali, NGOs na watanzania wote kwa ujumla.
Lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanaweza kupata huduma bora za kibenki kwa ufanisi Zaidi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege mara baada ya kutembelea banda la TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka akimkabidhi mkoba kutoka benki ya TIB Corporate mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea banda la Benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka mara baada ya kutembelea banda la benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka mara baada ya kutembelea banda la benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...