Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Mh. Mohamed Utaly ambaye alikuwaMgeni Rasmi katika
Hafla ya Kitaaluma iliyo ambatana na Shukrani pamoja pongezi kwa
mwanafunzi Bora kitaifa kidato cha Sita Bw. Anthony Mulokozi katika
Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Morogoro akitoa hotuba yake ambapo
alimpongeza Anthony Mulokozi kwa kufanya vizuri, pia aliwapongeza walimu
kwa kuendelea kuwa na juhudi za kuwafundisha wanafunzi kwa bidii na
mwisho alisema kuwa juhudi zote hizi za elimu bora zinatokana na
Serikali kuamua kulipa swala la elimu kipaumbele zaidi.

Mkuu
wa Shule ya Sekondari Mzumbe Bw. Wenceslaus Mushi akielezea malengo ya
Hafla hiyo ambayo ilikuwa ni ya kitaaluma zaidi na licha ya kuipongeza
na kutoa Shukurani kwa Serikali lakini pia alimpongeza Tanzania One
Anthony Mulokozi kwa kuwa Mwanafunzi Bora kidato cha sita kwa mwaka 2018
pamoja na wanafunzi wengine wote waliofanya vizuri pia aliwapongeza
walimu kwa kuendelea kuwa na bidii ya kuwafundisha wanafunzi kwa weredi.

Afisa
Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Mvomero Bw. Omat Sanga
akizungumza neno wakati wa hafla hiyo ya kitaaluma iliyo ambatana na
kutoa shukrani pamoja na pongezi katika Shule ya Sekondari Mzumbe .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...