WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Mameneja wa shirika la Umeme (Tanesco) kote nchini kuhakikisha wanakata huduma ya umeme kwa wadaiwa sugu ikiwemo sekta binafasi na serikalini. 

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Morogoro iliyokuwa na lengo la kutembelea maeneo yanayozalisha umeme ikiwemo Kidatu ambako uzalishaji wa umeme ni 204 mw. 

Licha ya kutembelea eneo hilo lakini pia alizindua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Alisema kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa kuweza kusaidia kukusanya madeni hayo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kukwamisha malengo yao waliojiwekea. 

Aidha alisema kwamba haiwezekani shirika hilo likawa linawadai watu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwenye kutekeleza shughuli za kimaendeleo na kuweza kuwafikia wananchi wengi huku wakiacha kuwachukulia hatua ambazo zinaweza kusaidia kupata ufumbuzi wake. 

“Ndugu zangu mameneja wa mikoa hakikisheni mnawakatia umeme wadaiwa wote sugu kwenye maeneo yenu wakiwemo wale wa sekta binafasi na serikali kwani hii ndio njia inayoweza kuwasaidia kukusanya madeni hayo “Alisema Dkt Kalemani. Akizungumzia kitengo cha huduma kwa wateja ndani ya shirika hilo Dkt Kalemani alisema ni muhimu watumishi wa kada hiyo wakabadilikana kitabia kwa sababu imedodira sana na kwenye maeneo mengi hazifanyi kazi zao ipasavyo. 
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo akishuhudia 
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kuzindua Rea awamu ya tatu
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt Kalemani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...