Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wiki mbili kwa vilabu vyote vya mchezo wa Kriketi nchini ambavyo havijasajiliwa kufika Baraza la Michezo La Taifa kwa ajili ya kujisajili .
Akizungumza na wadau hao wa mchezo huo jana katika Ukimbi wa mikutano uliopo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa ni wajibu wa kila kilabu cha mchezo nchini kufuata sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya michezo.
“Kama kuna kilabu chochote cha mchezo wa kikreti kipo na hakijasajiliwa, natoa wiki mbili kuweza kufuata taratibu na sheria za usajili ili viweze kutambulika kisheria ” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha aliongeza kwa kuutaka uongozi wa Chama cha Kriketi Tanzania kuhakikisha unatenga siku moja kwa ajili ya mkutano na wanachama wake ili kupata nafasi ya kupitia vipengele vinavyounda katiba ya chama hicho kwa ajili ya maboresho mbalimbali.
Vilevile Waziri Dkt. Mwakyembe alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali zinazokikabili chama hicho cha mchezo wa Kriketi na kuhaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Kwa Upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Makoye Nkenyenge amewataka wanachama hao kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Dkt. Mwakyembe kwa kuhakikisha wanasajili vilabu vyote ambavyo havijasajiliwa.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na wadau wa mchezo wa Kriketi alipokutana nao hapo jana katikati ukumbi wa mkutano uliopo Uwanja wa Taifa, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto) akieleza jambo kwa wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge (kulia) akizungumza na wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto).
Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania Bw. Taher Kitisa akizungumza wakati wa kikao kilichowahusisha wadau wa chama cha Kikreti pamoja na Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha), kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Kriketi ambaye pia ni Kocha wa mchezo huo Bw. Hussein Mohamedi akichangia jambo katika kikao kilichowahusisha wadau hao pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika Picha),katika kikao kilichofanyika jana uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...