Na Mathias Canal, NFRA
Zoezi la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula unaendelea katika maeneo mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito uliotolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.
Pamoja na Ubora wa mahindi kuwa changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana na hali ya msimu wa mwaka Jana kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa shambani.
Katika hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Octoba 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.
Katika ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi kufikia leo tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo imeshanunua zaidi ya tani 6000.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.
Afisa ubora wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Masanja akikagua mahindi kwenye kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...