Na mathias Canal-WK, Bariadi-Simiyu

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) leo Alhamisi Octoba 2018 amewataka wajasiriamali kote nchini kuchangamkia fursa ya kutembelea katika Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Katika maonesho hayo ambayo yalianza Oktoba 23 mwaka huu, Dkt Tizeba amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wananchi kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

"Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani kama Mara, Mwanza na Shinyanga wajitokeza kwa wingi kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa muhimu kwao katika kuakisi kwa vitendo Tanzania ya viwanda" Alisema Dkt Tizeba

Dkt Tizeba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa kubuni jambo hilo sambamba na kumpongeza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwa kuwaalika wajasiriamali, na wataalamu waoneshaji wa teknolojia mbalimbali kwani jambo hilo litatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

Aidha, Dkt Tizeba amesema kuwa Maonesho hayo ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao.Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO) yakiwa na Kauli Mbiu isemayo PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”. yalifunguliwa rasmi na Waziro Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo wakati akikagua mashine zinazotengenezwa na SIDO TDC kwa ajili ya uchakataji wa mazao mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...